Jumatatu, 30 Oktoba 2017

JINSI MATATIZO NA TAABU YANAVYO KUWA MSAADA WA MAFANIKO YAKO

Habari za leo ndugu?.  

Karibu kwenye makala yetu hii ya SARARI YA MAFANIKO ambapo leo tuta kwenda kujifunza jinsi taabu na shida zinavyo kuwa msaada mkubwa wa wewe kufanikiwa na kufikia hatima yako iliyo nzuri zaidi.

Kume kuwa na wimbi kubwa la watu wanaohitaji kufanikiwa katika maisha yao ambapo hutafuta kila namna ya kujinasua katika wimbi zito la umaskini. Katika makala hii leo naenda kukushirikisha jinsi taabu na shida zinavyo saidia kuimarisha mafanikio yako. Karibu ndugu tujifunze:-

     Taabu na shida, katika maisha ya Duniani ni lazima ukutane na taabu na shida, taabu na shida si kitu kibaya katika mafanikio yako bali ni mashine ya  kuimarisha na kusukuma ili ufikie unapo pataka . Watu wengi walio fanikiwa walisukumwa na taabu, shida na masimango kutoka kwa watu mbalimbali ambayo yaliwapa machungu ndani yao ya kuona sababu ya kutafuta mafanikio, taabu na shida huimarisha uwezo wa mtu kifikra na kujiweka tayari kupambana tofauti raha ambayo humfanya mtu adumae kifikra.

  Kutokana na taabu na shida jinsi zinavyo saidia katika mafanikio, leo nitaenda kutumia  mfano wa mti wa Mbuyu kama kielelezo cha mtu mwenye taabu na nitatumia Mpapai kama kielelezo cha mtu asiye na taabu. Mbuyu ni mti ambao huota pasipo uangalizi wowote, mti huu hujitegemea wenyewe, hua haumwagiliziwi maji wala mbolea haupatiwi yaani kwa kifupi Mbuyu ni mti usio tunzwa kabisa bali hujitunza wenyewe. Vile vile kuna mti wa Mpapai ambao wenyewe hutunzwa na kumwagiliwa maji huku ukiwekewa mbolea kila wakati unapo hitaji kwa lengo la kustawi vizuri, Mpapai hutuzwa kwa kiwango kikubwa sana.


                                                                  
     Tofauti ya Mpapai na Mbuyu huonekana katika uimara wake, ambapo mbuyu huonekana imara na mnene kutokana na wenyewe kujijegemea,  mizizi yake hupambana kwenda ardhini mbali zaidi kwa ajili ya kusaka maji hivyo kuufanya mbuyu uendelee kustawi na kuwa imara zaidi. Mpapai wenyewe hua na matunzo ambapo mizizi yake haiendi mbali zaidi katika ardhi kwasababu ya kutegemea maji  unao mwagiliziwa ya karibu ili uweze kustawi na kuendelea kuishi.

Tofauti ya hizi miti miwili ni pale ukame utakapo tokea au upepo mkali utakapo tokea, hapo ndo utatambua ni kipi kilicho imara zaidi. Ukweli ni kwamba upepo utakapo tokea mpapai huanguka haraka sana na ukame unapotokea Mpapai hukauka haraka sana tofauti na Mbuyu ambao haufi kizimbe au aukauki kizembe kutokana na mazingira ya taabu na shida ulimomkulia ambapo taabu na shida ziliufanya mti huu kuwa Imara zaidi.

Katika maisha maisha yako ya Mafanikio usiogope taabu na shida unazo kutana nazo bali imarika kupitia shida hizo na taabu hizo, unacho takiwa ni kumshuru Mungu aliye kupitisha katika shida hizo ili akufanye uimarike kama mbuyu.

Kamwe usikate tamaa kwa sababu ya masimango unayo kutatana nayo bali yatumie kama injini ya wewe kusonga mbele, kumbuka unakutana na hayo kwa sababu wewe ni Mbuyu unaye jitegemea kwa kila kitu, na kama wewe ni Mbuyu jitahidi sana usijifananishe na Mpapai ambao unatunzwa na mwisho wake wakati wa majanga huangamia haraka sana.

Waache wanao kucheka leo wakucheke, natambua wanakucheka kwa sababu wao ni Mpapai humwagiliziwa na kutuzwa kwa kupewa mbolea zaidi ili wazidi kustawi, wao ni tofauti na wewe ambae unajitafutia kila kitu, Kumbuka wao humwagiliziwa na kuangaliwa vizuri na hiki ndicho kiburi walicho nacho na wanasahau kwamba ipo siku wale wanao wamwagilizia wakizembea kuwamwagilizia na ukame ukitokea watakauka haraka sana.

Ndugu yangu sisemi uwe na utengano bali ninacho kiamini ni kwamba mtu anaye ishi kwa shida na taabu mwisho wake hua ni mziuri sana, na mwisho wake utakuwa mzuri pale tu atakapo piga hatua kuyatafuta mafanikio kama jinsi Mbuyu unavyo fanya. Kumbuka kuwa Mbuyu nao ungekuwa unapitia Taabu na shida na ukabaki palepale pasipo kupiga hatua usingeweza kuimarika, wenyewe hau haukati tamaa kutoka na mazingira bali huchua hatua ya kusaka maji kwa nguvu wakati wa ukame, na hivi ndivyo inavyo takiwa katika safari yako ya mafanikio, kuwa mtu wa kuyatafuta mafanio yalipo usikubali tu kupitia katika taabu na shida na hatimaye ukabali umetuliu tu bali piga hatua na kwa kufanya hivyo mafanikio yatakufuata.

Magumu yaweza kuwa na manufaa kwako endapo utayatumia kama mashine ya kukufikisha kule unako kutaka, watu wengi wanapitia taabu na shida lakini hawafanikiwi hii ni kutokana na na wao kuwa na machungu mengi lakini hawatafuti namna ya kufanikwa na hawaweki nguvu katika kufanikiwa. Ndugu yangu unatakiwa uyatumie mazingira yako ya magumu unayo yapitia kama njia sasa ya wewe kufukia hatima ya mafanikio kwa kufanya kazi kwa bidii huku ukiyatupilia mbali maneno ya wengi wanayo yasema.

Ukiwa mchapa kazi mwenye malengo mafanikio lazima yakufuate, hakuna aliye fanya kazi kwa bidii na kwa malengo akabaki maskini, sisemi ufanye kazi tu kisha uache bali unatakiwa ufanye kazi kwa bidii na kwa malengo. Taabu na shida zisikufanye unung'unike na kubaki umetulia mahali ilipo bali zitumie kupiga hatua kubwa zaidi na hatimaye unenepe na kuwa Imara kama Mbuyu ulivyo.


 Nakutakia safari njema ya mafaniko ndugu yangu.
               wako ndugu katika SAFARI YA MAFANIKIO,
                       Daniel Mbugu.



     Kwa mafundisho mengi zaidi yahusuyo mafaniko waweza kutembeleamy  BLOGU hii ya SAFARI YA MAFANIKIO.  Kwa ushauri zaidi juu ya mafundisho haya niliyo kushirikisha wasiliana nami katika www.danielmbuguj@gmail.com. au waweza tuma ujumbe mfupi kwenda namba 0655505173.


Jumapili, 13 Agosti 2017

JINSI FIKRA INAVYO FANYA KAZI KATIKA KUTENGENEZA MAFANIKIO YAKO.

Habari za leo ndugu?.  

Karibu kwenye makala yetu hii ya SARARI YA MAFANIKO ambapo leo tuta kwenda kujifunza jinsi fikra inavyo saidia katika kukutengenezea mafaniko yako. Kumekuwa na misemo mingi kuhusiana na mitazamo ya watu juu ya mafaniko, ambapo wengine wanadiliki kusema kuwa mafaniko ya mtu yategemeanana ukoo wake kwa maana hiyo wana kuwa wakimaanisha kuwa kama ukoo wako ni maskini na wewe utakuwa masikini tu na kama ukoo wako ni tajiri na wewe utakuwa ni tajiri.

Katika hili leo tunakwenda kuangalia jinsi Fikra inayo saidia katika kukufanikisha. 
Mafanikio ya mtu yeyote yule alie fanikiwa kwa nguvu zake ni lazima yalianza kujengwa katika Fikra zake. Kile aliocho kuwa amekiwaza ndicho alicho kuwa amekiweka katika matendo na akafikia mafanikio. Kumbuka maana ya mafanikio ni kutimiza malengo yako ulio kuwa umeyaweka, kwa maana hii namaanisha mafanikio si kupata fedha maana ingekuwa hivyo walio matajiri wasinge kuwa wanaangaika na fedha kwa sababu wanazo. Mafanikio ingekuwa kupata nyumba wengi wenye nyumba wesingekuwa wana taka kufanikiwa, bali mafanikio ni kutimiza malengo ambayo mtu anakuwa ameyaweka ndani ya Fikra zake ili ayatimize.
Kumbuka malengo ya mtu huanzia ndani ya Fikra , kama mtu ameweka malengo makubwa maana yake Fikra zake amezitengeneza katika kujengeka malengo makubwa na kama mtu anamalengo madogo maana yake Fikra zake zimetengeneza katika kuwajibika kwa malengo madogo.
Tofauti iliyopo kati ya watu walio fanikiwa na wale ambao hawaja fanikiwa ni katika mitazamo yao ya ndani ambayo imo katika Fikra. Walio fanikiwa wengi ukiwauliza ulifanyeje mpaka ukafanikiwa wengi wao utasikia wanasema nili fikiri kinyume na wengine. 

Katika maisha yako ya kutaka kufikia jambo flani unalo lipenda unatakiwa kufikiri kwa kina kuhusiana na kile unacho kihitaji. Fikra ni kitu chenye uhai wa kutenda,  katika mafanikio ya mtu kama unataka kuamini ninacho kwambia ebu  jichunguze wewe mwenyewe utagundua kuwa kile unacho kifanya ni chanzo cha kile ulicho kifikilia, hata kusoma makala hii ulianza katika Fikra na yamkini ulikuwa ukibishana na fikira zako kuhusiana na kuisoma ama kutoisoma. 
Ukwe ni kwamba mambo yote tunayo yahitaji katika mafanikio tunahitaji kubadili fikra zetu kutoka uduni na kuziweka ziwaze yale tunayo yahitaji.
      VITU VINAVYO SABABISHA MTU KUWA NA FIKRA ZA KUFANIKIWA AMA ZA KUTOFANIKIWA;-
  1. Elimu, katika maisha ya mwanadamu ya hapa Duniani hakuna mtu anaye ishi pasipo kuwa na elimu, elimu zaweza tofautina kutokana na mtu mwenyewe. Kwa mfano wewe unaye soma makala hii kama isingekuwa elimu uliyo ipata darasani usingeweza kusoma hapa , kwa hiyo elimu hii uliyo ipata imekusaidia mpaka sasa unakuwa na fikira za kisomi. Elimu anayo ipata mtu yaweza mumfanikisha au kumfanya asifanikiwe.      

Katika elimu yetu rasmi ya darasani ni mara chache sana kufundishwa habari za kuhusiana na matumizi ya feza au kuhusiana na uhalisia halisi wa ali za ugumu ulioko katika maisha ya mtaani, na mara nyingi wanao tufundisha huwa wanasema kuwa tusome ili tupate maisha mazuri, na pale mtu anapo maliza masomo yake na akakuta hakuna uhalisia wa alicho ambiwa hukuta anakata tamaa sana. Swali  linakujua kwanini anakata tamaa?,  jibu ni kwasababu Fikra zake zilibeba ujumbe alio jifunza ya kuwa baada ya masomo ni kupata maisha mazuri, na alivyo soma hajapata ajira na yuko sawa na yule aliye muacha mataani. 
Tatizo si ajira bali ni Fikra alizo zibeba kuhusina na elimu yake. 
Kama unataka kufanikiwa katika maisha haya ni lazima ubadili fikra zako kutoka kule ulikonasa kwa umaskini na uziweke katika mafanikio unayo hitaji kuya pata, maana kwa kufanya hivyo utabdilisha mtazamo wako wa maendeleo. Kumbuka fikra ndizo zilizo beba uwajibikaji, ukimujona mtu anawajibika sana katika kila jambo tambua kuwa fikra zake ameziwekea mtazamo wa kuwajibika.
             2. Watu wanao kuzunguka, watu wanao kuzunguka waweza kuubadili mwelekeo wako wa kimaisha kifikra. Kwa mfano kama wewe haukuwa na fikra za kuvuta Bangi na ukawana marafiki wengi wanao ipenda bangi na kuisififia ni lazima kuna siku na wewe utatamani ujaribu uwe kama wao uone kitu wanacho kipata, na kwa kufanya hivyo unajikuta unabadili fikra zako za msimao wa kupinga tabia hizo na ukaanza kutumia.
Ukitaka kuona uhalisia wa hili angalia marafiki 7 wa mtu flani ambao wameshibana sana , wengi utakuta tabia zao ziko sawa. Kwahiyo katika Marafiki au ndugu hapo ndipo tunajengewa tabia za umasikini ya kwamba unakuta mtu anaminishwa kataika kukata tamaa na Fikra yake inanasa na kuanza kuamini ndani ya moyo wake ya kuwa mafanikio ni katika ukooflani au katika watu falani. Ndugu msomaji nataka leo utambue kuwa mahali ulipo haikuja kwa sababu ya bahati mbaya au nzuri bali ni kutokana na kile kitu ulicho kuwa nacho katika Fikra zakao. Kumbuka kuwa ''kile unacho kitenda ni matokeo ya kile unacho kiwaza, kama ukiwaza vibaya utatenda vibaya na kama ukiwaza vizuri utatenda vizuri''
     3.Mazingira, mazingira yanayo kuzunguka yanaweza kukupa mtazamo flani wa kifikra. Kwa mfano kama mtu amekulia sehemu ya kisiwani ina maana jamii yake kubwa inakuwa imejikita katika uvuvi, na yeye kutokana na mazingira yake kuwa shupavu katika uvuvi hali hii inamjengea kuwa na fikra za kufikilia uvuvi tu kama chanzo cha mafanikio. Hawezi kutoka katika hilo wazo labda apate kitu cha kusoma au cha kusikia kitakacho mfanya atambue vitu vya tofauti na mazingira yake, kitu hicho kiki achilia mwanga ndani yake utamuona anaanza kubalili Msimamo na kuanza kufikri kinume na alivyo kuwa ameamini katika uvuvi tu.
Mafaniko ya mtu yamejificha katika kile anacho kiwaza, kama akiongeza bidii ya kuwajibika kufuata fikra ni lazima utafanikiwa. Fikra hubeba mambo yote yaani mabaya na mazuri pia, kwahiyo kama una fikra za kutenda mabaya utafanikiowa katika mabaya hayo, na kama una fikra za kutenda mambo mazuri utafanikiwa katika mambo hayo.

Ili uweze kufanikiwa katikia maisha yako kwa kutimiza ndoto zako, usipigane na watu wengine bali jenga fikfra za kukfanikisha. na fikra za mafanikio huwa zinajengwa na mambo mbalili

         VITU VINAVYO JENGA FIKRA ZA MAFANIKIO;-

  1. Kusoma, iliwe kubadili mtazamo wako wa kifikra unatakiwa kuwa msomaji wa vitun mbalimbali haswa vile unavyo vipenda kuvifikia. Katika maandiko ya vitabu ndiko tunako kutana na mawazo mbalimbali ya watu walio fanikiwa wakielezea fikra zao za kimafanikio ambazo zimewasaidia. Kumbuka ni ngumu sana kwa mtu kuongea kila kitu alicho kumbana nacho katika maisha yake ya mafanikio lakini katika maandisha naweza kuongea na wewe na kukupa ujuzi wa kusonga mbele katika mafanikio yako.
  2. Kusikiliza, ili uweze kubadili fikra zako za mwanzo za kiumasini unatakiwa kusikiliza shuhuda na mbinu mbalili za walio wafanikiwa maana watakutia moyo na watakuongezea mtazamo wa kifikra utakao kusaidia kufukia malengo yako uliyo yapanga. Katika kusikia kuna kuamini na katika kuamini kuna  imani na katika imani kuna msimamo ambao utakusidia kwenda kinyume na fikra za wanao kupinga . 

Ndugu msomaji tatizo la mafanikio liko kwako mwenyewe na kile unacho kisoma na kukisikiza, kumbuka unacho kiona na kukisikiliza kina kujengea uaminifu flani wa mafanio, penda kusikiliza na kusoma vitu vya mafanikio navyo vitakufanya ufanikiwe na kuwa bora zaidi katika fikra na katika mienendo maana "kile unacho kitenda ni matokeo tu ya kile anacho kiwaza" kwahiyo ukiwaza vibaya tegemea kuvuna mabaya na ukiwaza vizuri tegemea kuvuna mazuri.
Nakushauri ndugu yangu ubadili mtazamo wako wa kufikiri na ufikri kuwa wewe ni mshindi na mwenye mafanikio katika kile unacho kipenda, na baada ya kufikiria hivyo unatakiwa uweke malengo yako katika vitendo maana kufikri tu hakutoshi kukufanikisha bali matendo ya kile unacho kifikiri ndicho kitakupa mafanikio mazuri zaidi.
 Nakutakia safari njema ya mafaniko ndugu yangu.
               wako ndugu katika SAFARI YA MAFANIKIO,
                       Daniel Mbugu.



     Kwa mafundisho mengi zaidi yahusuyo mafaniko waweza kutembeleamy  BLOGU hii ya SAFARI YA MAFANIKIO.  Kwa ushauri zaidi juu ya mafundisho haya niliyo kushirikisha wasiliana nami katika www.danielmbuguj@gmail.com. au waweza tuma ujumbe mfupi kwenda namba 0758505174/0655505173.


Ijumaa, 14 Julai 2017

TABIA (4) ZINAZO KUFANYA USHINDWE KUPATA FEDHA NYINGI.


 Habari za leo ndugu?.  Vipi unaendeleaje na safari yako ya mafanikio?



Karibu kwenye makala yetu hii ya SARARI YA MAFANIKO ambapo leo tunaenda kuangalia tabia 4 ambazo ukizifanya zitakusababisha ushindwe kupata fedha za kutosha.
kumekuwa na changamoto nyingi za kuwatu kudai kwamba fedha walizo nazo hazitoshi na wengi wao wanasingizia ya kua yamkini wao wamezaliwa na mikosi au laana ili waishi kwa shida katika safari yao ya kutafuta mafaniko hapa Dunia.






              Ukweli nikwamba katika maisha ya duniani hakuna mtu ambaye amezaliwa ili asifanikwe katika kupata fedha nyingi, kama hakuna mtu ambaye amezaliwa ili asifanikwe kupata fedha nyingi maana yake ni kwamba kila aliye zaliwa ambaye anaishi katika Dunia hii kuna vitu ambavyo akivifuata vitamsababishia kupata fedha nyingi na kuna vitu ambavyo pia akivifuata vita msababishia kushidwa kupata fedha za kutosha.
                Ndugu msomaji, katika nakala hii tuta angalia tabia nne (4) ambazo ukizifanya zitakusababishia ushindwe kupata fedha nyingi. Tambua kwamba zipo tabia nyingi sana zinazo fanya wengi washindwe kufanikiwa lakini mimi leo naenda kukushirikisha tabia nne (4) tu. Tabia hizo ni zifuatazo:-
         1. Tabia ya kushindwa kuifanya fedha ikuzalishie fedha zingine, kama utakuwa na kitu ambacho hakikuzalishii tambua kitu hicho hakina faida kubwa kwako ingawa chaweza kuwa na faida lakini faida hiyo itakuwa ni kindogo kutokana na kwamba hakikuzalishii vitu vingine. Ndivyo ilivyo na katika suala la fedha, kama utakuwa na fedha ambayo haikuzalishii tambua hautopata fedha nyingi. kama kwa mwezi unaingiza kiasi cha tsh 80000 au zaidi je?  kiasi hicho unakitumia katika kuzalisha fedha nyingine?. Kama unacho halafu unaweka tu katika matumizi na hakikuzalishii tambua kabisa kuwa kiasi hicho hakitaongezeka na kwa maana hiyo kitapungua na kukusababishia kushindwa kupata fedha za kutosha. Ndugu msomaji kinacho takiwa ni kwamba unapo pata tu fedha wekeza kwenye fursa ambayo itakusababishia kukuza kipato ulicho nacho, haijalishi unapata fedha ndogo kiasi gani cha muhimu ni wewe kukitumia ili uweze kuzalisha zaidi na si kukitumia tu katika matumizi na kubaki unasubiria mpaka mwisho wa mwezi ndio upate kiasi kingine cha fedha.Unatakiwa uifanye fedha yako ikuzalishie fedha nyingine hatakama ni ndogo kiasi gani.
     2. Tabia ya kutothamini kile unacho kifanya, mara nyingi mafanikio ya kweli yanakuja kwa kukithamini kile unacho kifanya. Kwa mfano hapo ulipo waweza kuwa na kiasi flani cha fedha ambacho umekipata kutoka sehemu flani, unatakiwa uthamini kile kitu kinacho kusababishia wewe kupata fedha hiyo uliyo nayo, hakuna fedha inayo kuja pasipo kutoka kwenye chazo falani ambacho hua ni kazi aifanyayo mtu ambayo ni halali kiafya na kiserikali. Kwa hiyo kama hautoi thamani kubwa kwa kile unacho kifanya  utashindwa kutengeneza fedha nyingi,  kumbuka wengi ambao hawafanikiwi katika suala la fedha ni wale wanao ishi maisha ya mazoea na yakutothamini kile wanacho kifanya ambacho ndiyo nguzo kuu ya wao kupata fedha. Ndugu msomaji unatakiwa ujitofautishe na wao kwa maana watu wa tabia hizi kwao kufanikiwa hua ni ngumu sana, unacho takiwa kwako ni kuithamini na kuipenda kazi unayo ifanya. Kumbuka ili uwe mtu wa tofauti lazima ufanye mambo ya tofauti na ili uwe mtu wa kawaida unatikwa kufanya mabo ya kawaida, napenda kuku shauri ndugu yangu ya kuwa unatakiwa kuwa mtu wa tofauti na wale wasio ithamini kazi yao kwa kuithamini kazi yako, kwa kufanya hivyo utakuta unaingiza fedha nyingi sana.
        3.Tabia ya kufanya mambo kwa kawaida sana, sumu kubwa ya kuto fanikiwa na kutotengeneza kifedha nyingi ni kufanya mambo kwa kwaida kawaida. Watu wana mazoea ya kufanya kazi kwa kiwango cha kawaida huku wakitegemea kupata matokeo makubwa. Ili uweze kufanikiwa na kutengeneza fedha nyingi maishani mwako, jifunze kufanya kazi kwa bidii zote bila kuchoka, hii itakufanya uzidi kutengeneza mapato makubwa sana. Kama unazani natania katika hili angalia watu ambao siku zote maishani mwao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii huku wakiwa wanajifunza mambo yanayo husu kile wanacho kifanya. Watu hawa mara nyingi utakuta wanatengeneza fedha nyingi kutokana na kile wanacho kifanya kwa bidii na juhudi zao zote. 
               Kwahiyo moja yakitu kinacho kufanya ushindwe kutengeneza fedha nyingi sio mikosi au laana kama wengi wanavyo sema au kuzaliwa katika familia ya kipato cha chini kama wengi wanvyo laumu ya kuwa wamezaliwa familia ya kimasikini bali ni bidii yako ndogo ya kufanya mabo kwa kawaida. Kumbuka kama nilivyo kwisha kukwambia ya kwamba ili mtu tofauti unatakiwa ufanye mambo ya tofauti, na ili uwe wa kawaida fanya mambo ya kawaida na ili uwe wa chini fanya mabo ya chini. Ndungu msomaji katika nakala yetu hii ya SAFARI YA MAFANIKIO ninakusisitiza kufanya kazi kwa juhudi zako zote , ukifanya hivi baada ya miezi sita utakuwa umeona tofauti ya kipato na jinsi kinavyo ingia kwa kasi katika kile uacho kifaya. Ndugu msomaji Tambua kuwa kamwe bii hua hiendi hivi hivi bali huwa inafanya watu watimize malengo yao, wewe fanya tu bidii uone jinsi mambo yanavyo badilika na kuwa mazuri na yenye kupendeza. Naamini ukiongeza bidii katika kile unacho kifanya ipo siku utakuwa mtu wa kupata fedha nyingi na nzenye manufaa.
          4.Tabia ya kulidhika mapema, watu wengi wanakuwa na tabia ya kuridhika sana pale wapatapo mafaniko kidogo tu, huwa ni watu wa kulidhika na kuona kama wamekwisha kufika, hata zile juhudi walizo kuwa wakizifanya mwanzoni zinakuwa zinapotea kidogo kidogo kwa sababu ya mafaniko madogo waliyo yapata. Unapo kuwa na tabia hii tambua kuwa ni chanzo kikubwa kitakacho kufanya usifanikiwe katika safari yako ya kutengeneza fedha nyingi. Kwa mfano watu wengi wanapo kuwa wanatafuta mafaniko ya kupata elimu hua na mono ya kupata fedha nyingi kupitia elimu yao, lakini pale wanapo ajiliwa na kupa nyumba na gari huridhika na kuacha kujifunza jinsi ya kukitumia kipato walicho nacho katika kuwaingizia kipato kingiene, matokeo yake ni kwamba pale wanapo sitafu au pale wanapo achishwa kazi hukuta wanaishi maisha magumu sana kiasi cha kulingana na wale walio kuwa chini yao na muda mwingine walio chini yoa hukuta wanawapita kimaendeleo ya kifedha. Kumbuka kinacho wafanya waishi maisha magumu hayo ni tambia yao ya kuridhuika pindi walipo kuwa kazini. Wewe ndugu yangu unatakiwa uwe na kiu kubwa ya kuingiza fedha ambayo itakufanya ufanye kazi kwa bidii, kamwe usiridhike na kile unacho kifanya bali kitumie kukuongezea kipato kingine ili ufikie maisha ya mafaniko. kumbuka hakuna mtu alie zaliwa ili awe maskini bali tabia zako unazo zifanya ndizo zitakufanya ufanikiwe au usifanikiwe.
           Kwakuhitimisha napenda kukusihi Ndugu msomaji uyaepuke mambo ulio yasoma katika nakala hii fupi, usiyasome tu na kuyaacha bali yaweke katika vitendo maana kwa kufanya hivi utajikuta uningiza fedha nyingi na kuinua kipato chako ulicho nacho. Kumbuka kile kipato ulicho nacho chaweza kuongezeka na kuwa kikubwa zaidi na hivyo kukufanya upate fedha nyingi. Kumbuka nguvu kubwa aifanyayo mtu katika kutafuta mafaniko ya kifedha hua haipotei bali huweza kumwinua mtu kutoka sehemu ya chini na kwenda juu.
        Nakutakia safari njema ya mafaniko ndugu yangu.
               wako ndugu katika SAFARI YA MAFANIKIO,
                       Daniel Mbugu.


     Kwa mafundisho mengi zaidi yahusuyo mafaniko waweza kutembeleamy  BLOGU hii ya SAFARI YA MAFANIKIO.  Kwa ushauri zaidi juu ya mafundisho haya niliyo kushirikisha wasiliana nami katika www.danielmbuguj@gmail.com. au waweza tuma ujumbe mfupi kwenda namba 0758505174/0655505173.


JINSI MATATIZO NA TAABU YANAVYO KUWA MSAADA WA MAFANIKO YAKO

Habari za leo ndugu?.   Karibu kwenye makala yetu hii ya  SARARI YA MAFANIKO   ambapo leo tuta kwenda kujifunza jinsi taabu na shida zi...