Habari za leo ndugu?. Vipi unaendeleaje na safari yako ya mafanikio?
![]() |
kumekuwa na changamoto nyingi za kuwatu kudai kwamba fedha walizo nazo hazitoshi na wengi wao wanasingizia ya kua yamkini wao wamezaliwa na mikosi au laana ili waishi kwa shida katika safari yao ya kutafuta mafaniko hapa Dunia.
Ukweli nikwamba katika maisha ya duniani hakuna mtu ambaye amezaliwa ili asifanikwe katika kupata fedha nyingi, kama hakuna mtu ambaye amezaliwa ili asifanikwe kupata fedha nyingi maana yake ni kwamba kila aliye zaliwa ambaye anaishi katika Dunia hii kuna vitu ambavyo akivifuata vitamsababishia kupata fedha nyingi na kuna vitu ambavyo pia akivifuata vita msababishia kushidwa kupata fedha za kutosha.
Ndugu msomaji, katika nakala hii tuta angalia tabia nne (4) ambazo ukizifanya zitakusababishia ushindwe kupata fedha nyingi. Tambua kwamba zipo tabia nyingi sana zinazo fanya wengi washindwe kufanikiwa lakini mimi leo naenda kukushirikisha tabia nne (4) tu. Tabia hizo ni zifuatazo:-
1. Tabia ya kushindwa kuifanya fedha ikuzalishie fedha zingine, kama utakuwa na kitu ambacho hakikuzalishii tambua kitu hicho hakina faida kubwa kwako ingawa chaweza kuwa na faida lakini faida hiyo itakuwa ni kindogo kutokana na kwamba hakikuzalishii vitu vingine. Ndivyo ilivyo na katika suala la fedha, kama utakuwa na fedha ambayo haikuzalishii tambua hautopata fedha nyingi. kama kwa mwezi unaingiza kiasi cha tsh 80000 au zaidi je? kiasi hicho unakitumia katika kuzalisha fedha nyingine?. Kama unacho halafu unaweka tu katika matumizi na hakikuzalishii tambua kabisa kuwa kiasi hicho hakitaongezeka na kwa maana hiyo kitapungua na kukusababishia kushindwa kupata fedha za kutosha. Ndugu msomaji kinacho takiwa ni kwamba unapo pata tu fedha wekeza kwenye fursa ambayo itakusababishia kukuza kipato ulicho nacho, haijalishi unapata fedha ndogo kiasi gani cha muhimu ni wewe kukitumia ili uweze kuzalisha zaidi na si kukitumia tu katika matumizi na kubaki unasubiria mpaka mwisho wa mwezi ndio upate kiasi kingine cha fedha.Unatakiwa uifanye fedha yako ikuzalishie fedha nyingine hatakama ni ndogo kiasi gani.
2. Tabia ya kutothamini kile unacho kifanya, mara nyingi mafanikio ya kweli yanakuja kwa kukithamini kile unacho kifanya. Kwa mfano hapo ulipo waweza kuwa na kiasi flani cha fedha ambacho umekipata kutoka sehemu flani, unatakiwa uthamini kile kitu kinacho kusababishia wewe kupata fedha hiyo uliyo nayo, hakuna fedha inayo kuja pasipo kutoka kwenye chazo falani ambacho hua ni kazi aifanyayo mtu ambayo ni halali kiafya na kiserikali. Kwa hiyo kama hautoi thamani kubwa kwa kile unacho kifanya utashindwa kutengeneza fedha nyingi, kumbuka wengi ambao hawafanikiwi katika suala la fedha ni wale wanao ishi maisha ya mazoea na yakutothamini kile wanacho kifanya ambacho ndiyo nguzo kuu ya wao kupata fedha. Ndugu msomaji unatakiwa ujitofautishe na wao kwa maana watu wa tabia hizi kwao kufanikiwa hua ni ngumu sana, unacho takiwa kwako ni kuithamini na kuipenda kazi unayo ifanya. Kumbuka ili uwe mtu wa tofauti lazima ufanye mambo ya tofauti na ili uwe mtu wa kawaida unatikwa kufanya mabo ya kawaida, napenda kuku shauri ndugu yangu ya kuwa unatakiwa kuwa mtu wa tofauti na wale wasio ithamini kazi yao kwa kuithamini kazi yako, kwa kufanya hivyo utakuta unaingiza fedha nyingi sana.
3.Tabia ya kufanya mambo kwa kawaida sana, sumu kubwa ya kuto fanikiwa na kutotengeneza kifedha nyingi ni kufanya mambo kwa kwaida kawaida. Watu wana mazoea ya kufanya kazi kwa kiwango cha kawaida huku wakitegemea kupata matokeo makubwa. Ili uweze kufanikiwa na kutengeneza fedha nyingi maishani mwako, jifunze kufanya kazi kwa bidii zote bila kuchoka, hii itakufanya uzidi kutengeneza mapato makubwa sana. Kama unazani natania katika hili angalia watu ambao siku zote maishani mwao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii huku wakiwa wanajifunza mambo yanayo husu kile wanacho kifanya. Watu hawa mara nyingi utakuta wanatengeneza fedha nyingi kutokana na kile wanacho kifanya kwa bidii na juhudi zao zote.
Kwahiyo moja yakitu kinacho kufanya ushindwe kutengeneza fedha nyingi sio mikosi au laana kama wengi wanavyo sema au kuzaliwa katika familia ya kipato cha chini kama wengi wanvyo laumu ya kuwa wamezaliwa familia ya kimasikini bali ni bidii yako ndogo ya kufanya mabo kwa kawaida. Kumbuka kama nilivyo kwisha kukwambia ya kwamba ili mtu tofauti unatakiwa ufanye mambo ya tofauti, na ili uwe wa kawaida fanya mambo ya kawaida na ili uwe wa chini fanya mabo ya chini. Ndungu msomaji katika nakala yetu hii ya SAFARI YA MAFANIKIO ninakusisitiza kufanya kazi kwa juhudi zako zote , ukifanya hivi baada ya miezi sita utakuwa umeona tofauti ya kipato na jinsi kinavyo ingia kwa kasi katika kile uacho kifaya. Ndugu msomaji Tambua kuwa kamwe bii hua hiendi hivi hivi bali huwa inafanya watu watimize malengo yao, wewe fanya tu bidii uone jinsi mambo yanavyo badilika na kuwa mazuri na yenye kupendeza. Naamini ukiongeza bidii katika kile unacho kifanya ipo siku utakuwa mtu wa kupata fedha nyingi na nzenye manufaa.
4.Tabia ya kulidhika mapema, watu wengi wanakuwa na tabia ya kuridhika sana pale wapatapo mafaniko kidogo tu, huwa ni watu wa kulidhika na kuona kama wamekwisha kufika, hata zile juhudi walizo kuwa wakizifanya mwanzoni zinakuwa zinapotea kidogo kidogo kwa sababu ya mafaniko madogo waliyo yapata. Unapo kuwa na tabia hii tambua kuwa ni chanzo kikubwa kitakacho kufanya usifanikiwe katika safari yako ya kutengeneza fedha nyingi. Kwa mfano watu wengi wanapo kuwa wanatafuta mafaniko ya kupata elimu hua na mono ya kupata fedha nyingi kupitia elimu yao, lakini pale wanapo ajiliwa na kupa nyumba na gari huridhika na kuacha kujifunza jinsi ya kukitumia kipato walicho nacho katika kuwaingizia kipato kingiene, matokeo yake ni kwamba pale wanapo sitafu au pale wanapo achishwa kazi hukuta wanaishi maisha magumu sana kiasi cha kulingana na wale walio kuwa chini yao na muda mwingine walio chini yoa hukuta wanawapita kimaendeleo ya kifedha. Kumbuka kinacho wafanya waishi maisha magumu hayo ni tambia yao ya kuridhuika pindi walipo kuwa kazini. Wewe ndugu yangu unatakiwa uwe na kiu kubwa ya kuingiza fedha ambayo itakufanya ufanye kazi kwa bidii, kamwe usiridhike na kile unacho kifanya bali kitumie kukuongezea kipato kingine ili ufikie maisha ya mafaniko. kumbuka hakuna mtu alie zaliwa ili awe maskini bali tabia zako unazo zifanya ndizo zitakufanya ufanikiwe au usifanikiwe.
Kwakuhitimisha napenda kukusihi Ndugu msomaji uyaepuke mambo ulio yasoma katika nakala hii fupi, usiyasome tu na kuyaacha bali yaweke katika vitendo maana kwa kufanya hivi utajikuta uningiza fedha nyingi na kuinua kipato chako ulicho nacho. Kumbuka kile kipato ulicho nacho chaweza kuongezeka na kuwa kikubwa zaidi na hivyo kukufanya upate fedha nyingi. Kumbuka nguvu kubwa aifanyayo mtu katika kutafuta mafaniko ya kifedha hua haipotei bali huweza kumwinua mtu kutoka sehemu ya chini na kwenda juu.
Nakutakia safari njema ya mafaniko ndugu yangu.
wako ndugu katika SAFARI YA MAFANIKIO,
Daniel Mbugu.
Kwa mafundisho mengi zaidi yahusuyo mafaniko waweza kutembeleamy BLOGU hii ya SAFARI YA MAFANIKIO. Kwa ushauri zaidi juu ya mafundisho haya niliyo kushirikisha wasiliana nami katika www.danielmbuguj@gmail.com. au waweza tuma ujumbe mfupi kwenda namba 0758505174/0655505173.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni