Habari za leo ndugu?.
Karibu kwenye makala yetu hii ya SARARI YA MAFANIKO ambapo leo tuta kwenda kujifunza jinsi fikra inavyo saidia katika kukutengenezea mafaniko yako. Kumekuwa na misemo mingi kuhusiana na mitazamo ya watu juu ya mafaniko, ambapo wengine wanadiliki kusema kuwa mafaniko ya mtu yategemeanana ukoo wake kwa maana hiyo wana kuwa wakimaanisha kuwa kama ukoo wako ni maskini na wewe utakuwa masikini tu na kama ukoo wako ni tajiri na wewe utakuwa ni tajiri.
Katika hili leo tunakwenda kuangalia jinsi Fikra inayo saidia katika kukufanikisha.
Mafanikio ya mtu yeyote yule alie fanikiwa kwa nguvu zake ni lazima yalianza kujengwa katika Fikra zake. Kile aliocho kuwa amekiwaza ndicho alicho kuwa amekiweka katika matendo na akafikia mafanikio. Kumbuka maana ya mafanikio ni kutimiza malengo yako ulio kuwa umeyaweka, kwa maana hii namaanisha mafanikio si kupata fedha maana ingekuwa hivyo walio matajiri wasinge kuwa wanaangaika na fedha kwa sababu wanazo. Mafanikio ingekuwa kupata nyumba wengi wenye nyumba wesingekuwa wana taka kufanikiwa, bali mafanikio ni kutimiza malengo ambayo mtu anakuwa ameyaweka ndani ya Fikra zake ili ayatimize.
Kumbuka malengo ya mtu huanzia ndani ya Fikra , kama mtu ameweka malengo makubwa maana yake Fikra zake amezitengeneza katika kujengeka malengo makubwa na kama mtu anamalengo madogo maana yake Fikra zake zimetengeneza katika kuwajibika kwa malengo madogo.
Tofauti iliyopo kati ya watu walio fanikiwa na wale ambao hawaja fanikiwa ni katika mitazamo yao ya ndani ambayo imo katika Fikra. Walio fanikiwa wengi ukiwauliza ulifanyeje mpaka ukafanikiwa wengi wao utasikia wanasema nili fikiri kinyume na wengine.
Katika maisha yako ya kutaka kufikia jambo flani unalo lipenda unatakiwa kufikiri kwa kina kuhusiana na kile unacho kihitaji. Fikra ni kitu chenye uhai wa kutenda, katika mafanikio ya mtu kama unataka kuamini ninacho kwambia ebu jichunguze wewe mwenyewe utagundua kuwa kile unacho kifanya ni chanzo cha kile ulicho kifikilia, hata kusoma makala hii ulianza katika Fikra na yamkini ulikuwa ukibishana na fikira zako kuhusiana na kuisoma ama kutoisoma.
Ukwe ni kwamba mambo yote tunayo yahitaji katika mafanikio tunahitaji kubadili fikra zetu kutoka uduni na kuziweka ziwaze yale tunayo yahitaji.
VITU VINAVYO SABABISHA MTU KUWA NA FIKRA ZA KUFANIKIWA AMA ZA KUTOFANIKIWA;-
- Elimu, katika maisha ya mwanadamu ya hapa Duniani hakuna mtu anaye ishi pasipo kuwa na elimu, elimu zaweza tofautina kutokana na mtu mwenyewe. Kwa mfano wewe unaye soma makala hii kama isingekuwa elimu uliyo ipata darasani usingeweza kusoma hapa , kwa hiyo elimu hii uliyo ipata imekusaidia mpaka sasa unakuwa na fikira za kisomi. Elimu anayo ipata mtu yaweza mumfanikisha au kumfanya asifanikiwe.
Katika elimu yetu rasmi ya darasani ni mara chache sana kufundishwa habari za kuhusiana na matumizi ya feza au kuhusiana na uhalisia halisi wa ali za ugumu ulioko katika maisha ya mtaani, na mara nyingi wanao tufundisha huwa wanasema kuwa tusome ili tupate maisha mazuri, na pale mtu anapo maliza masomo yake na akakuta hakuna uhalisia wa alicho ambiwa hukuta anakata tamaa sana. Swali linakujua kwanini anakata tamaa?, jibu ni kwasababu Fikra zake zilibeba ujumbe alio jifunza ya kuwa baada ya masomo ni kupata maisha mazuri, na alivyo soma hajapata ajira na yuko sawa na yule aliye muacha mataani.
Tatizo si ajira bali ni Fikra alizo zibeba kuhusina na elimu yake.
Kama unataka kufanikiwa katika maisha haya ni lazima ubadili fikra zako kutoka kule ulikonasa kwa umaskini na uziweke katika mafanikio unayo hitaji kuya pata, maana kwa kufanya hivyo utabdilisha mtazamo wako wa maendeleo. Kumbuka fikra ndizo zilizo beba uwajibikaji, ukimujona mtu anawajibika sana katika kila jambo tambua kuwa fikra zake ameziwekea mtazamo wa kuwajibika.
2. Watu wanao kuzunguka, watu wanao kuzunguka waweza kuubadili mwelekeo wako wa kimaisha kifikra. Kwa mfano kama wewe haukuwa na fikra za kuvuta Bangi na ukawana marafiki wengi wanao ipenda bangi na kuisififia ni lazima kuna siku na wewe utatamani ujaribu uwe kama wao uone kitu wanacho kipata, na kwa kufanya hivyo unajikuta unabadili fikra zako za msimao wa kupinga tabia hizo na ukaanza kutumia.
Ukitaka kuona uhalisia wa hili angalia marafiki 7 wa mtu flani ambao wameshibana sana , wengi utakuta tabia zao ziko sawa. Kwahiyo katika Marafiki au ndugu hapo ndipo tunajengewa tabia za umasikini ya kwamba unakuta mtu anaminishwa kataika kukata tamaa na Fikra yake inanasa na kuanza kuamini ndani ya moyo wake ya kuwa mafanikio ni katika ukooflani au katika watu falani. Ndugu msomaji nataka leo utambue kuwa mahali ulipo haikuja kwa sababu ya bahati mbaya au nzuri bali ni kutokana na kile kitu ulicho kuwa nacho katika Fikra zakao. Kumbuka kuwa ''kile unacho kitenda ni matokeo ya kile unacho kiwaza, kama ukiwaza vibaya utatenda vibaya na kama ukiwaza vizuri utatenda vizuri''
3.Mazingira, mazingira yanayo kuzunguka yanaweza kukupa mtazamo flani wa kifikra. Kwa mfano kama mtu amekulia sehemu ya kisiwani ina maana jamii yake kubwa inakuwa imejikita katika uvuvi, na yeye kutokana na mazingira yake kuwa shupavu katika uvuvi hali hii inamjengea kuwa na fikra za kufikilia uvuvi tu kama chanzo cha mafanikio. Hawezi kutoka katika hilo wazo labda apate kitu cha kusoma au cha kusikia kitakacho mfanya atambue vitu vya tofauti na mazingira yake, kitu hicho kiki achilia mwanga ndani yake utamuona anaanza kubalili Msimamo na kuanza kufikri kinume na alivyo kuwa ameamini katika uvuvi tu.
Mafaniko ya mtu yamejificha katika kile anacho kiwaza, kama akiongeza bidii ya kuwajibika kufuata fikra ni lazima utafanikiwa. Fikra hubeba mambo yote yaani mabaya na mazuri pia, kwahiyo kama una fikra za kutenda mabaya utafanikiowa katika mabaya hayo, na kama una fikra za kutenda mambo mazuri utafanikiwa katika mambo hayo.
Ili uweze kufanikiwa katikia maisha yako kwa kutimiza ndoto zako, usipigane na watu wengine bali jenga fikfra za kukfanikisha. na fikra za mafanikio huwa zinajengwa na mambo mbalili
VITU VINAVYO JENGA FIKRA ZA MAFANIKIO;-
- Kusoma, iliwe kubadili mtazamo wako wa kifikra unatakiwa kuwa msomaji wa vitun mbalimbali haswa vile unavyo vipenda kuvifikia. Katika maandiko ya vitabu ndiko tunako kutana na mawazo mbalimbali ya watu walio fanikiwa wakielezea fikra zao za kimafanikio ambazo zimewasaidia. Kumbuka ni ngumu sana kwa mtu kuongea kila kitu alicho kumbana nacho katika maisha yake ya mafanikio lakini katika maandisha naweza kuongea na wewe na kukupa ujuzi wa kusonga mbele katika mafanikio yako.
- Kusikiliza, ili uweze kubadili fikra zako za mwanzo za kiumasini unatakiwa kusikiliza shuhuda na mbinu mbalili za walio wafanikiwa maana watakutia moyo na watakuongezea mtazamo wa kifikra utakao kusaidia kufukia malengo yako uliyo yapanga. Katika kusikia kuna kuamini na katika kuamini kuna imani na katika imani kuna msimamo ambao utakusidia kwenda kinyume na fikra za wanao kupinga .
Nakushauri ndugu yangu ubadili mtazamo wako wa kufikiri na ufikri kuwa wewe ni mshindi na mwenye mafanikio katika kile unacho kipenda, na baada ya kufikiria hivyo unatakiwa uweke malengo yako katika vitendo maana kufikri tu hakutoshi kukufanikisha bali matendo ya kile unacho kifikiri ndicho kitakupa mafanikio mazuri zaidi.
Nakutakia safari njema ya mafaniko ndugu yangu.
wako ndugu katika SAFARI YA MAFANIKIO,
Daniel Mbugu.
Kwa mafundisho mengi zaidi yahusuyo mafaniko waweza kutembeleamy BLOGU hii ya SAFARI YA MAFANIKIO. Kwa ushauri zaidi juu ya mafundisho haya niliyo kushirikisha wasiliana nami katika www.danielmbuguj@gmail.com. au waweza tuma ujumbe mfupi kwenda namba 0758505174/0655505173.