Jumatatu, 30 Oktoba 2017

JINSI MATATIZO NA TAABU YANAVYO KUWA MSAADA WA MAFANIKO YAKO

Habari za leo ndugu?.  

Karibu kwenye makala yetu hii ya SARARI YA MAFANIKO ambapo leo tuta kwenda kujifunza jinsi taabu na shida zinavyo kuwa msaada mkubwa wa wewe kufanikiwa na kufikia hatima yako iliyo nzuri zaidi.

Kume kuwa na wimbi kubwa la watu wanaohitaji kufanikiwa katika maisha yao ambapo hutafuta kila namna ya kujinasua katika wimbi zito la umaskini. Katika makala hii leo naenda kukushirikisha jinsi taabu na shida zinavyo saidia kuimarisha mafanikio yako. Karibu ndugu tujifunze:-

     Taabu na shida, katika maisha ya Duniani ni lazima ukutane na taabu na shida, taabu na shida si kitu kibaya katika mafanikio yako bali ni mashine ya  kuimarisha na kusukuma ili ufikie unapo pataka . Watu wengi walio fanikiwa walisukumwa na taabu, shida na masimango kutoka kwa watu mbalimbali ambayo yaliwapa machungu ndani yao ya kuona sababu ya kutafuta mafanikio, taabu na shida huimarisha uwezo wa mtu kifikra na kujiweka tayari kupambana tofauti raha ambayo humfanya mtu adumae kifikra.

  Kutokana na taabu na shida jinsi zinavyo saidia katika mafanikio, leo nitaenda kutumia  mfano wa mti wa Mbuyu kama kielelezo cha mtu mwenye taabu na nitatumia Mpapai kama kielelezo cha mtu asiye na taabu. Mbuyu ni mti ambao huota pasipo uangalizi wowote, mti huu hujitegemea wenyewe, hua haumwagiliziwi maji wala mbolea haupatiwi yaani kwa kifupi Mbuyu ni mti usio tunzwa kabisa bali hujitunza wenyewe. Vile vile kuna mti wa Mpapai ambao wenyewe hutunzwa na kumwagiliwa maji huku ukiwekewa mbolea kila wakati unapo hitaji kwa lengo la kustawi vizuri, Mpapai hutuzwa kwa kiwango kikubwa sana.


                                                                  
     Tofauti ya Mpapai na Mbuyu huonekana katika uimara wake, ambapo mbuyu huonekana imara na mnene kutokana na wenyewe kujijegemea,  mizizi yake hupambana kwenda ardhini mbali zaidi kwa ajili ya kusaka maji hivyo kuufanya mbuyu uendelee kustawi na kuwa imara zaidi. Mpapai wenyewe hua na matunzo ambapo mizizi yake haiendi mbali zaidi katika ardhi kwasababu ya kutegemea maji  unao mwagiliziwa ya karibu ili uweze kustawi na kuendelea kuishi.

Tofauti ya hizi miti miwili ni pale ukame utakapo tokea au upepo mkali utakapo tokea, hapo ndo utatambua ni kipi kilicho imara zaidi. Ukweli ni kwamba upepo utakapo tokea mpapai huanguka haraka sana na ukame unapotokea Mpapai hukauka haraka sana tofauti na Mbuyu ambao haufi kizimbe au aukauki kizembe kutokana na mazingira ya taabu na shida ulimomkulia ambapo taabu na shida ziliufanya mti huu kuwa Imara zaidi.

Katika maisha maisha yako ya Mafanikio usiogope taabu na shida unazo kutana nazo bali imarika kupitia shida hizo na taabu hizo, unacho takiwa ni kumshuru Mungu aliye kupitisha katika shida hizo ili akufanye uimarike kama mbuyu.

Kamwe usikate tamaa kwa sababu ya masimango unayo kutatana nayo bali yatumie kama injini ya wewe kusonga mbele, kumbuka unakutana na hayo kwa sababu wewe ni Mbuyu unaye jitegemea kwa kila kitu, na kama wewe ni Mbuyu jitahidi sana usijifananishe na Mpapai ambao unatunzwa na mwisho wake wakati wa majanga huangamia haraka sana.

Waache wanao kucheka leo wakucheke, natambua wanakucheka kwa sababu wao ni Mpapai humwagiliziwa na kutuzwa kwa kupewa mbolea zaidi ili wazidi kustawi, wao ni tofauti na wewe ambae unajitafutia kila kitu, Kumbuka wao humwagiliziwa na kuangaliwa vizuri na hiki ndicho kiburi walicho nacho na wanasahau kwamba ipo siku wale wanao wamwagilizia wakizembea kuwamwagilizia na ukame ukitokea watakauka haraka sana.

Ndugu yangu sisemi uwe na utengano bali ninacho kiamini ni kwamba mtu anaye ishi kwa shida na taabu mwisho wake hua ni mziuri sana, na mwisho wake utakuwa mzuri pale tu atakapo piga hatua kuyatafuta mafanikio kama jinsi Mbuyu unavyo fanya. Kumbuka kuwa Mbuyu nao ungekuwa unapitia Taabu na shida na ukabaki palepale pasipo kupiga hatua usingeweza kuimarika, wenyewe hau haukati tamaa kutoka na mazingira bali huchua hatua ya kusaka maji kwa nguvu wakati wa ukame, na hivi ndivyo inavyo takiwa katika safari yako ya mafanikio, kuwa mtu wa kuyatafuta mafanio yalipo usikubali tu kupitia katika taabu na shida na hatimaye ukabali umetuliu tu bali piga hatua na kwa kufanya hivyo mafanikio yatakufuata.

Magumu yaweza kuwa na manufaa kwako endapo utayatumia kama mashine ya kukufikisha kule unako kutaka, watu wengi wanapitia taabu na shida lakini hawafanikiwi hii ni kutokana na na wao kuwa na machungu mengi lakini hawatafuti namna ya kufanikwa na hawaweki nguvu katika kufanikiwa. Ndugu yangu unatakiwa uyatumie mazingira yako ya magumu unayo yapitia kama njia sasa ya wewe kufukia hatima ya mafanikio kwa kufanya kazi kwa bidii huku ukiyatupilia mbali maneno ya wengi wanayo yasema.

Ukiwa mchapa kazi mwenye malengo mafanikio lazima yakufuate, hakuna aliye fanya kazi kwa bidii na kwa malengo akabaki maskini, sisemi ufanye kazi tu kisha uache bali unatakiwa ufanye kazi kwa bidii na kwa malengo. Taabu na shida zisikufanye unung'unike na kubaki umetulia mahali ilipo bali zitumie kupiga hatua kubwa zaidi na hatimaye unenepe na kuwa Imara kama Mbuyu ulivyo.


 Nakutakia safari njema ya mafaniko ndugu yangu.
               wako ndugu katika SAFARI YA MAFANIKIO,
                       Daniel Mbugu.



     Kwa mafundisho mengi zaidi yahusuyo mafaniko waweza kutembeleamy  BLOGU hii ya SAFARI YA MAFANIKIO.  Kwa ushauri zaidi juu ya mafundisho haya niliyo kushirikisha wasiliana nami katika www.danielmbuguj@gmail.com. au waweza tuma ujumbe mfupi kwenda namba 0655505173.


JINSI MATATIZO NA TAABU YANAVYO KUWA MSAADA WA MAFANIKO YAKO

Habari za leo ndugu?.   Karibu kwenye makala yetu hii ya  SARARI YA MAFANIKO   ambapo leo tuta kwenda kujifunza jinsi taabu na shida zi...